Zaha aanza kulazimisha kutua Chelsea - Darajani 1905

Zaha aanza kulazimisha kutua Chelsea

Share This

Winga wa Crystal Palace, Wilfred Zaha ambaye ni raia wa Uingereza amekataa kusaini mkataba mpya wa kusalia klabuni hapo na inaelezwa kwamba ameshawaaga wachezaji wenzake kwamba anaondoka.

Nyota huyo anatakiwa na klabu ya Chelsea na kuna taarifa zinasema amewaaga wachezaji wenzake akiwa na lengo la kukamilisha usajili wake wa kutua Chelsea.

Lakini kusalia kwa Willian Borges klabuni Chelsea ambaye ameshaanza mazoezi kunaweza kufifiisha usajili wa nyota huyo kutua Chelsea ambapo hapo kabla ilipangwa Willian angeondoka Chelsea basi klabu hiyo ingemfata Zaha kama mrithi wa Willian.

No comments:

Post a Comment