Rasmi; Pedro kuzeekea Chelsea - Darajani 1905

Rasmi; Pedro kuzeekea Chelsea

Share This

Winga na mshambuliaji wa Chelsea, Pedro Rodriguez amesaini mkataba mpya klabuni hapo ambapo ataitumikia mpaka mwaka 2020.

Pedro ambaye ameifungia Chelsea magoli mawili katika michezo mitatu ya kirafiki amesaini mkataba huo hii leo zikiwa zimepita siku kadhaa toka atimize miaka 31.

Mataji kadhaa aliyoyashinda akiwa Chelsea ni pamoja na ligi kuu Uingereza, Kombe la FA na Kombe la ligi.

No comments:

Post a Comment