Kumbe hii ndiyo sababu iliyomfanya Loftus-Cheek kurejea mapema Chelsea, kocha Sarri kufanya maamuzi - Darajani 1905

Kumbe hii ndiyo sababu iliyomfanya Loftus-Cheek kurejea mapema Chelsea, kocha Sarri kufanya maamuzi

Share This

Kutokana na michuano ya Kombe la Dunia kuchezeka mwaka huu basi wale wachezaji walioshiriki michuano hiyo walipewa muda wao wa kupumzika tofauti na wake ambao hawakushiriki michuano hiyo na muda huo wa kupumzika hutegemea na nafasi ambayo timu yako imefikia kwenye michuano hiyo.

Kama timu yako iliishia hatua ya makundi basi hiyo inamaanisha utapumzika mapema kuliko yule ambaye timu yake imefika hatua ya mbele.

Hivyo klabu ya Chelsea ilitoa tarehe za kila mchezaji kurejea klabuni ili kujiandaa na msimu mpya.

Lakini kwanini kiungo wa Chelsea, Ruben Loftus-Cheek amerejea mapema kuliko nyota wengine waliofikia hatua ya kumtafuta mshindi wa tatu ambao ni Gary Cahill, Michy Batshuayi, Eden Hazard na Thibaut Courtois?

Kumbe sababu inayoelezwa iliyomfanya kiungo huyo kurejea mapema ni kujiweka sawa na akihitaji kupata nafasi katika kikosi cha Chelsea ambacho kwasasa kipo chini ya kocha Maurizio Sarri.

Inaelezwa kwamba nyora huyo aliyerejea klabuni siku ya juzi jumatano badala ya kurejea kesho kutwa jumapili kama alivyopangiwa anahitaji kuelewa mfumo wa kocha huyo mpya ili aweze kumshawishi kocha Sarri ampe nafasi kwenye msimu wake mpya.

Inaelezwa pia kama kocha huyo hatomtumia kiungo huyo basi kuna uwezekano nyota huyo akalazimisha kuondoka.

Msimu uliopita aliutumia akiwa kwa mkopo kwenye klabu ya Crystal Palace ambako huko kulimfanya akajumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza na kufanikiwa kuichezea michezo minne kwenye Kombe la Dunia.

No comments:

Post a Comment