Morata abadili namba, aikimbia laana ya namba 9 - Darajani 1905

Morata abadili namba, aikimbia laana ya namba 9

Share This

Tarehe 29-Julai ni siku ya kumbukumbu kubwa kwa mshambuliaji nyota wa klabu ya Chelsea, Alvaro Morata ambapo amekiri akisema familia yake kwake ni jambo kubwa sana na ndio maana akaamua kubadilisha namba yake ya jezi kutoka namba 9 ya mwanzo mpaka namba 29 ambayo inawakilisha tarehe ambayo alifanikiwa kushuhudia familia yake na mkewe Alice Campello ikipata watoto wawili mapacha.

Nyota huyo anasema kupata watoto hao kwake ni jambo kubwa hivyo kuamua kutumia tarehe 29 kama namba ya jezi yake klabuni Chelsea.

Lakini wakati hilo linatokea, tukio hilo la kubadili namba linahusishwa pia kwamba amekimbia laana ya namba ya jezi namba 9 klabuni Chelsea.

Inadhaniwa kwamba karibu kila mchezaji ambaye amewai kuitumia namba hiyo akiwa klabuni Chelsea basi huwa ni ngumu kwake kucheza kwa kiwango kikubwa kama Morata alivyokuwa akilalamikiwa kutokana na ubutu wake kwenye kufumani nyavu.

Takwimu zinaonyesha toka mmiliki wa klabu, Roman Abramovich ameinunua klabu hiyo mwaka 2003, ni mchezaji mmoja tu aliyevaa jezi namba 9 klabuni Chelsea aliyefunga magoli zaidi ya 50, ni Jimmy Hasselbaink pekee aliyefanya hivyo ambaye toka mwaka 2000 mpaka mwaka 2004 alifunga magoli 88

Takwimu hizi hapa;
2000-04: Jimmy Floyd Hasselbaink
Alisajiliwa akitokea: Atletico Madrid
Ada ya usajili: £15m
Michezo aliyocheza Chelsea: 177
Magoli: 88

2004-05: Mateja Kezman
Alisajiliwa akitokea: PSV
Ada ya usajili: £5m
Michezo aliyocheza Chelsea: 41
Magoli : 7

2005-06: Hernan Crespo
Alisajiliwa akitokea: Inter
Ada ya usajili: £16.8m
Michezo aliyocheza Chelsea: 73
Magoli : 25

2006-07: Khalid Boulahrouz
Alisajiliwa akitokea: Hamburg
Ada ya usajili: £8.5m
Michezo aliyocheza Chelsea: 20
Magoli : 0

2007-08: Steve Sidwell
Alisajiliwa akitokea: Reading
Ada ya usajili: Bure
Michezo aliyocheza Chelsea: 25
Magoli : 1

2008-09: Franco Di Santo
Alisajiliwa akitokea: Audax Italiano
Ada ya usajili: £3.4m
Michezo aliyocheza Chelsea: 16
Magoli : 0

2011-14: Fernando Torres
Alisajiliwa akitokea: Liverpool
Ada ya usajili: £50m
Michezo aliyocheza Chelsea: 172
Magoli : 45

2015-16: Radamel Falcao
Alisajiliwa akitokea: Monaco
Ada ya usajili: Mkopo
Michezo aliyocheza Chelsea: 12
Magoli : 1

2017-18-: Alvaro Morata
Alisajiliwa akitokea: Real Madrid
Ada ya usajili: £70m
Michezo aliyocheza Chelsea: 48
Magoli : 15

No comments:

Post a Comment