Wakala wa Courtois azidi kupigilia misumari - Darajani 1905

Wakala wa Courtois azidi kupigilia misumari

Share This

Mlinda mlango wa Chelsea, Thibaut Courtois kwasasa yupo nchini Hispania ambako huko amefika ili kuitembelea familia yake ya watoto wawili lakini uku familia yake ikitajwa kuwa sababu kwake kutaka kujiunga na klabu ya Real Madrid ili asalie na familia yake.

Hilo pia limethibitishwa na wakala wa nyota huyo ambapo alipoulizwa mustakabali wa mlinda mlango huyo kama ni kubaki au kuondoka Chelsea, wakala huyo alisema "Nimesoma kwamba Chelsea imesema maamuzi ni yake lakini inaeleweka kwamba yeye anataka kujiunga na Real Madrid ili awe karibu na familia yake. Hilo ni jambo la muhimu kwake".

Courtois amebakiza mkataba wa mwaka mmoja klabuni Chelsea, mkataba unaomalizika mwaka 2019 huku Chelsea ikiwa na hofu ya kulazimika kumuuza kabla ya kuondoka bure atakapomaliza mkataba wake.

No comments:

Post a Comment