Morata awataja wachezaji bora klabuni Chelsea - Darajani 1905

Morata awataja wachezaji bora klabuni Chelsea

Share This

Jana ilikuwa siku nyengine tamu kwa nyota wa Chelsea, Alvaro Morata ambaye alitambulisha rasmi kuanza kuvaa jezi namba 29 kuanzia msimu huu ambapo maamuzi hayo ameyafanya ili kuonyesha kwa kiasi gani amefurahishwa na ujio wa watoto wake mapacha ambao wamezaliwa siku ya tarehe 29-Julai. Mwanzoni mshambuliaji huyo alikuwa akivaa jezi namba 9.

Mara baada ya utambulisho huo, nyota huyo akafanyiwa mahojiano na chombo kimoja cha habari na kati ya maswali aliyoulizwa ni kuhusu wachezaji waratu anaodhani wamefanya vizuri katika michezo mitatu ambayo Chelsea imecheza ili kujiandaa na msimu mpya. Michezo hiyo ni ule dhidi ya Perth Glory, dhidi ya Inter Milan na dhidi ya Arsenal.

Nyota huyo aliwataja Callum Hudson-Odoi, Ethan Ampadu na Jorginho Frello.

"Sijawai kumuona mchezaji aliyekuwa bora kama yeye (Callum Hudson-Odoi), ukiangalia umri wake na anayoyafanya ni mambo mawili tofauti. Nafikiri ana bahati sana kwa kuwa yupo klabu moja na wachezaji bora kama Eden (Hazard) na Willian. Kama akiwasikiliza kile wanachomweleza na akazingatia basi atakuwa mchezaji mkubwa sana"

"Yeye (Callum Hudson-Odoi) na Ampadu huwa wananishangaza sana, ukiwaangalia wanavyocheza unaweza kusema wana miaka 25 au 26, lakini kumbe ndiyo kwanza wana miaka 17"

"Nafikiri tuna bahati sana kumpata mchezaji bora kama yeye (Jorginho). Anaonyesha uthubutu na uwezo wa hali ya juu. Jambo zuri ni kwamba tulifanikiwa kumpata lakini lingekuwa jambo baya kama Manchester city wangefanikiwa kumnasa badala ya sisi" alisema Morata akimzungumzia Jorginho.

No comments:

Post a Comment