Kocha Sarri awaongelea Hazard, Courtois na Willian - Darajani 1905

Kocha Sarri awaongelea Hazard, Courtois na Willian

Share This

Jana kulichezeka mchezo wa kirafiki kati ya Chelsea dhidi ya Arsenal, mchezo ulioisha kwa sare ya 1-1 kabla ya Arsenal kuondoka na ushindi uliopatikana katika upigaji wa penati. Arsenal wakipata ushindi wa 6-5 katika hatua hiyo ya matuta au penati.

Mara baada ya mchezo huo kumalizika, kocha Maurizio Sarri wa Chelsea alifanyiwa mahojiano kuhusu kinachoendelea klabuni Chelsea kwasasa.

Hapa nakuletea baadhi ya mambo aliyoyazungumza

"Sijui kama hajiamini. Labda itakuwa alichoka sana, siku tatu zilizopita zilikuwa zimembana sana lakini kwa upande wangu, sina wasiwasi nae" alisema kocha huyo akizungumzia  kiwango cha Alvaro Morata

"Kwa muda huu siwezi kuzungumza chochote kwasababu nategemea kukutana nao siku ya jumamosi" alisema kocha Sarri alipoulizwa kuhusu Courtois na Eden Hazard wanaohusishwa kutaka kuondoka Chelsea.

"Nahitaji kuzungumza nae kwanza kabla sijalijibu swali hili. Sijafurahishwa na jambo hili lakini ni lazima nizungumze naye" alisema kocha Sarri alipoulizwa kuhusu kuchelewa kwa Willian kurejea klabuni.

No comments:

Post a Comment