Willian arejea Chelsea, aanza mazoezi - Darajani 1905

Willian arejea Chelsea, aanza mazoezi

Share This

Winga wa Chelsea, Willian Borges da Silva amerejea rasmi klabuni Chelsea akitokea kwenye mapumziko aliyopewa kutokana na kushiriki michuano ya Kombe la Dunia aliyoshiriki akiwa na timu yake ya taifa.

Nyota huyo mwenye miaka 29 ilitakiwa arejee klabuni siku ya tarehe 28-Julai lakini kutokana na matatizo ya kibali cha kusafiria (passport) yakamfanya kushindwa kuripoti klabuni kwa muda aliopangiwa na klabu hivyo klabu ikampatia muda wa nyongeza ili aweke mambo sawa na hivyo kumwambia ilitakiwa arejee klabuni tarehe 1-Agosti ambayo ndo ilikuwa jana.

Hatimaye nyota huyo amerejea klabuni akifikia kwenye uwanja wa mazoezi wa Chelsea, Cobham na kuanza mazoezi marahisi ili kujiweka sawa kutokana na kutoka kwenye likizo.

Nyota waliorejea mpaka sasa;
Kenneth Omeruo
Victor Moses
Antonio Rudiger
Cesar Azpilicueta
Andreas Christensen
Willy Caballero
Ruben Loftus-Cheek
Willian Borges

Nyota ambao bado hawajarejea:
Gary Cahill
Eden Hazard
Michy Batshuayi
Thibaut Courtois
Olivier Giroud
N'Golo Kante

No comments:

Post a Comment