Chelsea yapoteza kwa matuta, pata uchambuzi kutoka kwa YokoYoko King - Darajani 1905

Chelsea yapoteza kwa matuta, pata uchambuzi kutoka kwa YokoYoko King

Share This

Usiku wa jana kuamkia leo, klabu ya Chelsea ilicheza mchezo wake wa tatu wa kujinoa na kujiweka sawa kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu na michuano mingine ambapo kwa Chelsea itacheza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu siku ya tarehe 11-Agosti dhidi ya Huddersfield.

Mchezo huo wa jana ulichezwa huko jijini Dublin nchini Jamhuri ya Ireland kwenye uwanja wa nne kwa ukubwa nchini humo, uwanja wa Aviva ikicheza dhidi ya watani wao kutokea jiji la London, Arsenal ambapo mchezo huo uliisha kwa Chelsea kupoteza kwenye matuta 6-5.

Kwenye dakika 90' za mchezo ulimalizika kwa sare ya 1-1 ambapo goli la Chelsea lilifungwa na mlinzi raia wa Ujerumani, Antonio Rudiger aliyeonganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Cesc Fabregas na kuifanya Chelsea kupata goli la kuongoza katika dakika ya 5' wakati goli la Arsenal likifungwa katika dakika za majeruhi.

YokoYoko King
Chelsea inaonekana kumiliki vyema mchezo huku ikitengeneza mashambulizi mengi lakini tatizo linaonekana bado katika safu ya ushambuliaji. Magoli matatu katika michezo mitatu sio jambo jema katika kupambania ubingwa katika michuano ambayo Chelsea inashiriki.

Lakini pia inaonekana kocha Maurizio Sarri alipanga kuutumia mchezo huu ili kuamua kikosi kitakachocheza mchezo ujao dhidi ya Manchester city katika mchezo wa Ngao ya Hisani. Kocha huyo aliwatoa wachezaji wote walioanza katika mchezo huo na kuwaingiza nyota wengine 11.

Simuoni Alvaro Morata ambaye kocha Sarri anamuhitaji. Nadhani kuna mshambuliaji mpya atasajiliwa kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

Mchezo unaofata
Chelsea vs Manchester city
Siku; Tarehe 5-Agosti
Muda; Saa 05:00 Jioni (Saa 17:00) kwa saa za Afrika Mashariki
Michuano; Ngao ya Hisani

No comments:

Post a Comment