PL; FT, CHELSEA 2-0 BRIGHTON, MORATA ASHANGILIA KUMSUBIRI MTOTO - Darajani 1905

PL; FT, CHELSEA 2-0 BRIGHTON, MORATA ASHANGILIA KUMSUBIRI MTOTO

Share This
Furaha imerudi Chelsea, furaha imerudi tena Darajani, furaha imerudi tena The Blues

Alvaro Morata na Marcos Alonso wamehusika vyema kuirudisha furaha hiyo klabuni Chelsea mara ya jioni ya leo kuiongoza vyema klabu hiyo kupata ushindi wa muhimu ulioifanya kupunguza pengo la alama kati yake na Manyumbu (Manchester united) kutoka alama 3 mpaka alama 1 mara baada ya Manyumbu hao kunusurika kufungwa wakiwa kwao ambapo iliwahitaji dakika 90+5' kupata sare ya 2-2.

Mabingwa watetezi, Chelsea iliutawala mchezo katika kipindi cha kwanza ila haikufanikiwa kuzifumania nyavu ila katika kipindi cha pili wale mapacha raia wa nchi moja yaani Alvaro Morata na Cesar Azpilicueta Tanco wakafanya yao mara baada ya kama kawaida Cesar akitimiza pasi yake ya goli (assist) akiwa nazo 6 kwa sasa akapiga krosi tamu iliyomfikia vyema Alvaro Morata na nyota huyo kufunga kama kawaida yake kwa kichwa.

Kwa 'assist' hiyo inamfanya Cesar Azpilicueta kutimiza pasi za mabao 6 ambazo zote amempasia Alvaro Morata na kumfanya Morata kutimiza magoli 10 kwenye ligi kuu huku Cesar Azpilicueta akiwa mlinzi aliyetoa pasi nyingi za mabao.

Baada ya goli hilo, Alvaro Morata alishangilia tena kwa kuweka kidole mdomoni kuonyesha kuwa na hamu kubwa na mtoto wake ambapo kwa sasa mke wake ana mimba ila ambapo alifanya hivyo katika mchezo wa kombe la ligi dhidi ya Bournemouth kwa kuweka mpira ndani ya fulana na kuadhibiwa kwa kupewa kadi ya njano iliyomfanya kukosa mchezo mmoja. Anaonekana kumtamani sana mtoto wake.

Goli jengine lilifungwa na Marcos Alonso aliyefunga kwa kichwa akipokea krosi tamu iliyopigwa kwa mpira wa kona na kuutumia mpira huo kuiandikia Chelsea bao la pili, kona ikipigwa na Cesc Fabregas.

Kwa matokeo hayo, Chelsea inasalia nafasi ya tatu ingawa safari hii imepunguza pengo la alama na kuzidi kuisogelea Manyumbu inayoshika nafasi ya pili.

*Asanteni Chelsea, hivi ndivyo tunavyotaka mashabiki wetu muwe, ushindi wenu kwetu ni raha tupu, mnatufanya tutambe
My Blood, is totally Blue
Asante Mungu

No comments:

Post a Comment