Chelsea leo inashuka tena uwanjani ikiwa zimepita siku mbili toka kucheza mchezo wake wa ligi dhidi ya Everton mchezo ulioisha kwa sare ya 0-0 huku Chelsea ikiutawala mchezo huo kwa kiasi kikubwa.
Chelsea katika mchezo wa leo itashuka uwanjani kumenyana ana Brighton ambapo itataka alama tatu za muhimu katika mchezo huo huku nyota wake Alvaro Morata atakuwa analejea katika mchezo huu mara baada ya kukosekana katika mchezo dhidi ya Everton kutokana na kuwa na adhabu iliyomfanya kukosa mchezo mmoja.
Kikosi kinachotabiriwa kucheza leo dhidi ya Brighton ni pamoja na Thibaut Cortois akiwa kama kipa golini, Cesar Azpilicueta akicheza kama mlinzi wa kati ila anayekaa kushoto yaani Right-Centre Back (RCB), Andreas Christensen ambaye anakuwa kama mlinzi wa kati yaani Centre Back (CB), Antonio Rudiger aliyecheza pia katika mchezo liopita dhidi ya Everton ambapo yeyea atacheza kama mlinzi wa kati anayetokea upande wa kushoto yaani Left-Centre Back (LCB) huku katikati akiwepo Tiemoue Bakayoko ambaye amekuwa akionekana kuanza kufanya vizuri mara baada ya kuanza vibaya atakuwa kama kiungo mkabaji yaani Defensive Midfilder (DMF) huku [ia N'Golo Kante ambaye amechaguliwa kuwa mchzaji bora wa Ufaransa kwa mwaka 2017 akicheza pia kama kiungo mkabaji yaani Defensive Midfilder (DMF) na kwa upande wa mkono wa kulia akiwepo Victor Moses akiwa kama Winga wa kulia anayecheza pia kama mlinzi wa kulia yaani Right-Wing Back (RWB) wakati Marcos Alonso akiwa kama winga wa kushoto anayecheza pia kama mlinzi wa kushoto yaani Left-Wing Back (LWB) wakati kwa upande wa washambuliaji akiwepo Eden Hazard, Alvaro Morata pamoja na Willian Borges.
Mchezo huo utachezwa saa 12:00 Jioni.
PL; KIKOSI CHA CHELSEA vs BRIGHTON, LEO JIONI
Share This
Tags
# Chelsea HD
Share This
About Darajani 1905
Chelsea HD
Labels:
Chelsea HD
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment