M/Kirafiki: Habari muhimu kuelekea Arsenal vs Chelsea - Darajani 1905

M/Kirafiki: Habari muhimu kuelekea Arsenal vs Chelsea

Share This

Kwenye uwanja wa Aviva wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 57,100 huko jijini Dublin nchini Jamhuri ya Ireland usiku wa leo kutazikutanisha klabu mbili kutoka jijini London pale Uingereza, Chelsea dhidi ya Arsenal kwenye mchezo wa kirafiki katika mfululizo wa michezo ya ICC.

Kuelekea kwenye mchezo huo utakaochezwa saa 10:05 usiku (saa 22:05) kwa saa za Afrika Mashariki, hapa nakuletea habari muhimu kuhusu mchezo huo.

Kuhusu mchezo
Huu ni mchezo unaowakutanisha makocha wapya kwenye klabu zao mpya tena zikiwa zinatokea jiji moja la London na tena wakishiriki ligi kuu ngumu ya Uingereza na usisahau kwamba makocha wote hii ni mara ya kwanza kwao kufundisha timu za Uingereza. Ni Maurizio Sarri kwa Chelsea dhidi ya Unai Emery wa Arsenal.

Chelsea
Chelsea itashuka kwenye mchezo huu uku ikiwa na nyota waliorejea wakitokea kwenye michuano ya Kombe la Dunia na kufanikiwa kuanza mazoezi wakiongozwa na nahodha msaidizi Cesar Azpilicueta. Bado safu ya ushambuliaji itaendelea kuongozwa na Alvaro Morata, Pedro na Tammy Abraham ambao wao watakuwa kama washambuliaji pekee kwenye kikosi cha wachezaji 23 waliochaguliwa kushiriki mchezo huo.

Kikosi kinaweza kuanza kwenye mchezo huo;
Marcin Bulka, Cesar Azpilicueta, David Luiz, Ethan Ampadu, Marcos Alonso, Jorginho, Cesc Fabregas, Ross Barkley, Pedro, Hudson-Odoi na Alvaro Morata (mfumo: 4-3-3)

Arsenal
Wametoka kupata ushindi kwenye mchezo uliopita dhidi ya PSG, ushindi wa mabao 5-1 lakini faida waliyokuwa nayo ni wachezaji wake wengi wapo muda mrefu wakiwa pamoja kutokana na kutoshiriki michuano ya Kombe la Dunia.

Rekodi
Katika mchezo wa mwisho ambao timu hizo zimemenyana katika mchezo wa kirafiki uliisha kwa Chelsea kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Muda
Saa 10:05 Usiku (Saa 22:05) kwa saa za Afrika Mashariki

No comments:

Post a Comment