LIVER WAMNYAKUA DIJK - Darajani 1905

LIVER WAMNYAKUA DIJK

Share This

Klabu ya Liverpunga (Liverpool) imefanikiwa kuinasa saini ya nyota na mlinzi wa klabu ya Southampton, Virgil van Dijk ambaye ni raia wa Uholanzi kwa dau lililoweka rekodi mpya katika ligi kuu Uingereza.

Van Dijk amesajiliwa kwa kiasi cha paundi milioni 75 ambacho ni kiasi sawa na alichosajiliwa Romelu Lukaku kutoka Everton kwenda Manyumbu (Man united) ambao wote kwa ujumla wameweka rekodi ya wachezaji waliosajiliwa ndani ya Uingereza kwa dau kubwa.

Van Dijk mwenyewe ameshamalizana kila kitu na Liverpunga au wazee wa kale ambapo mlinzi huyo atapokea mshahara wa paundi 200,000 kwa wiki.

No comments:

Post a Comment