Luis Enrique apuuzia maneno ya Wenger, akaribia Chelsea - Darajani 1905

Luis Enrique apuuzia maneno ya Wenger, akaribia Chelsea

Share This

Gazeti la nchini Hispania limetoa ripoti likidai kocha wa zamani wa Barcelona, Luis Enrique anakaribia kuwa kocha wa Chelsea licha ya kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kudai anatamani kocha huyo atue Arsenal pindi ye atakapoachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Taarifa zinadai kuwa kocha huyo ameshafanya mazungumzo na moja ya viongozi kwenye klabu hiyo ya washika bunduki ambaye kiongozi huyo aliwai kuwa moja ya viongozi wa Barcelona lakini mazungumzo hayo hayakufikia muafaka na sasa anatajwa kuachana na mpango wa kujiunga na Arsenal na anatazamia kutua Chelsea kuchukua nafasi ya kocha wa sasa, Antonio Conte.

Antonio Conte anatajwa kutokuwa na muda mrefu wa kuwa kocha wa Chelsea na tayari makocha washatajwa kuchukua nafasi ya kocha huyo ambaye hata kama akifanikiwa kushinda taji la kombe la FA ambapo fainali itachezwa mwezi ujao bado haitofanya msimu kuwa mzuri kwa Chelsea.

No comments:

Post a Comment