Kocha Antonio Conte anatajwa kutokua na maisha marefu ya kuendelea kusalia kuwa kocha wa klabu ya Chelsea licha ya kubakiza
mwaka mmoja kwenye mkataba ambao aliusaini upya msimu uliopita mara baada ya kuipatia taji la ligi kuu katika msimu wake wa kwanza toka alipotua mwaka 2016.
Maelewano mabaya kati yake na bodi ya Chelsea yanatajwa kuwa chanzo kikubwa kinachomfanya kocha huyo kutokua na maisha marefu klabuni hapo lakini pia kushindwa kulitetea taji la ligi kuu na kutokua na msimu mzuri ndizo sababu zinazohusishwa kuendelea kutafuna maisha ya kocha huyo na sasa kuna makocha baadhi wanatajwa kuwaniwa na Chelsea ili kurithi nafasi ya mwalimu huyo raia wa Italia.
Kati ya makocha wanatajwa kuwaniwa na klabu hiyo ni pamoja na kocha wa klabu ya Tottenham, Mauricio Pochettino ambaye hatajwi sana kutakiwa na Chelsea ila vyanzo baadhi kutoka Uingereza vinalitaja jina lake kuwemo kwenye majina ya makocha wanaotakiwa na Chelsea.
No comments:
Post a Comment