Chelsea yapeleka maombi ya kumsajili Salah - Darajani 1905

Chelsea yapeleka maombi ya kumsajili Salah

Share This

Alisajiliwa na Chelsea mwaka 2014 akitokea FC Basel, lakini hakufanikiwa kupata nafasi zaidi kwenye kikosi kilichochini ya kocha Jose Mourinho ambapo alipata nafasi ya kucheza michezo 19 tu kabla ya baadae kutolewa kwa mkopo kisha kuuzwa kwenye klabu ya nchini Italia, As Roma. Ni Mohammed Salah, kwa sasa anaichezea Liverpool huku akionyesha uwezo mkubwa ambapo mpaka sasa ameshaichezea klabu hiyo michezo 47 na kuifungia magoli 43.

Chombo cha habari cha nchini Hispania maarufu kama Diario Gol kinadai Chelsea imepeleka maombi kwa nyota huyo ili arejee Chelsea.

Chelsea inatajwa na chombo hicho kuwa imepeleka maombi kwa nyota huyo ili arejee tena Chelsea licha ya kushindwa kupata nafasi kwenye kikosi hicho miaka minne iliyopita.

Kocha wake wa Liverpool, Jurgen Klopp aliwai kuhojiwa juu ya anadhani kwanini nyota huyo aliyeshinda tunzo ya mchezaji bora wa mwaka alishindwa kung'aa akiwa Chelsea. Kusoma alichokisema, bonyeza hapa

No comments:

Post a Comment