Klabu ya Chelsea iliwai kumsajili winga raia wa Misri akitokea klabu ya FC Basel, Mohammed Salah ambaye juzi alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka akiwa anaichezea klabu ya Liverpool ambapo nyota huyo hakufanikiwa kwenye maisha yake ya soka klabuni Chelsea akiichezea michezo 13 na kuifungia magoli mawili kabla ya kutolewa kwa mkopo kwenda Fiorentina kabla ya baadae kuuzwa kabisa.
Mafanikio aliyoyapata tangu aondoke klabuni Chelsea kunamfanya kocha Jose Mourinho (ambaye ndiye alikuwa kocha wa Chelsea kipindi iko) kupokea malalamiko makubwa kwa kushindwa kukitumia kipaji cha nyota huyo, kocha wake wa sasa klabuni Liverpool, Jurgen Klopp amejitokeza na kueleza kilichomfanya Salah ashindwe kung'aa kwenye kikosi cha Chelsea lakini pia akimtetea Mourinho juu ya nyota huyo.
"Nadhani (Salah) alishindwa kung'aa akiwa Chelsea ni kutokana na umri wake kuwa mdogo pindi akiwa kule, lakini pia kutokana na ukubwa na uimara wa kikosi cha Chelsea kwa kipindi iko"
"De Bruyne pia alishindwa kufanya vizuri, yote ni kutokana na ubora wa Chelsea uliokuwa nao kipindi iko. Lakini hakuna anayebisha kuwa Mourinho ni kocha bora, naamini ilikuwa ngumu kwake kuwapa nafasi Salah na De Bruyne kutokana na ubora uliokuwepo Chelsea kwa kipindi iko" alisema Jurgen Klopp.
Je unaamini hiyo ni kweli? au Mourinho anastahili kulaumiwa?
No comments:
Post a Comment