Nyota wa Chelsea atwaa tena tunzo nyengine - Darajani 1905

Nyota wa Chelsea atwaa tena tunzo nyengine

Share This

Nyota wa kikosi cha soka la wanawake cha Chelsea maarufu kama Chelsea Ladies, Fran Kirby amefanikiwa kutwaa tunzo nyengine ya mchezaji bora mwaka kwa ligi kuu Uingereza maarufu kama FWA ambayo hutolewa na chama cha wanawake waandishi wa soka nchini Uingereza.

Fran Kirby amechaguliwa kushinda tunzo hiyo ikiwa ni tunzo yake ya pili kama mchezaji binafsi mara baada ya jumapili iliyopita kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka kwa ligi kuu Uingereza kwa soka la wanawake, tunzo iliyotolewa na chama cha wanasoka wa kulipwa maarufu kama PFA.

Fran Kirby amekuwa msaada mkubwa na muhimili imara kwenye kikosi cha Chelsea Ladies msimu huu mara baada ya kuiongoza kufikia hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa barani Ulaya lakini pia akiiongoza klabu hiyo kuongoza kwenye msimamo wa ligi kuu ya wanawake ya nchini Uingereza huku mwenyewe akifunga magoli mawili.

No comments:

Post a Comment