Bakayoko, Morata wagombaniwa sokoni, Chelsea yapata kigugumizi - Darajani 1905

Bakayoko, Morata wagombaniwa sokoni, Chelsea yapata kigugumizi

Share This

Klabu ya Chelsea inatajwa kuwa tayari kupokea ofa ya nyota wake Tiemoue Bakayoko na mshambuliaji Alvaro Morata wanaoonekana kushindwa kuwa bora na kuwa bora tangu watue Chelsea kwenye dirisha kubwa la usajili lililopita.

Wachezaji hao walioigharimu Chelsea paundi milioni 100 kusajiliwa katika dirisha hilo la mwaka 2017 wamekuwa wakilalamikiwa na mashabiki wengi wa Chelsea kuwa wameshindwa kuwa bora na hawajaziba mapengo ya walioondoka ambapo kwa nafasi ya kiungo, Bakayoko anaonekana kushindwa kuziba pengo la Nemanja Matic aliyetimkia Manchester united wakati Alvaro Morata akionekana kushindwa kuziba pengo la Diego Costa.

Bakayoko anatajwa kutakiwa na klabu yake ya As Monaco iliyomuuza kuja Chelsea wakati Alvaro Morata akitakiwa na Juventus ambayo aliwai kuichezea. Lakini bodi ya Chelsea inatajwa kukubali kuwauza wachezaji hao kama wakishindwa kung'aa kwenye msimu ujao.

No comments:

Post a Comment