Wachezaji wa Chelsea watengeneza rekodi mpya - Darajani 1905

Wachezaji wa Chelsea watengeneza rekodi mpya

Share This

Nyota vijana wa Chelsea ambao wanacheza kwa mkopo kwenye klabu kadhaa barani Ulaya wamefanikiwa kutengeneza rekodi mpya ya kuzichezea klabu zao wanazozichezea kwa mkopo kwa dakika 74,000 toka kujiunga na klabu hizo kwa majira tofauti, lakini kwa takwimu hizo ni kwa msimu huu. Chelsea imewatoa kwa mkopo wachezaji 37.

Ethan Baxter ndiye anaongoza kupata nafasi ya kuichezea kwa muda mrefu klabu ya Woking FC ambayo ameichezea kwa dakika 4,230 huku nyota anayefata akiwa ni Ola Aina anayeichezea Hull city, mpaka sasa ameshaichezea kwa dakika 3,831.

Hii ni rekodi mpya inawekwa kwa wachezaji na makinda wa Chelsea katika kufikia rekodi hiyo huku wakijinoa vyema ili kuitumikia klabu pendwa ya Chelsea.

No comments:

Post a Comment