Napoli waitajia Chelsea dau la Koulibaly - Darajani 1905

Napoli waitajia Chelsea dau la Koulibaly

Share This

Chelsea imekuwa ikitajwa kuifukuzia saini ya nyota raia wa Senegal, Kalidou Koulibaly kwa muda mrefu sasa. Toka mwaka 2016 Chelsea imekuwa ikijaribu kuipata saini ya mlinzi huyo wa kati lakini kulitokea kauzibe hatimaye dili hilo likashindikana kukamilika.

Lakini sasa kunaelezwa huenda usajili huo ukakamilika katika dirisha kubwa la usajili linalokuja haswa kutokana na gazeti la nchini Italia ambapo ndipo anapoitumikia klabu yake ya Napoli kuripoti kuwa klabu hiyo ipo tayari kumuuza msenegal huyo endapo itatokea klabu itakayotoa paundi milioni 60 ili kumsajili.

Koulibaly mwenye uwezo mkubwa wa Chelsea anaweza akasajiliwa na klabu hiyo ya nchini Uingereza lakini Darajani 1905 inaamini wa mchezaji huyo unashinikizwa na kocha mkuu, Antonio Conte na kama ikitokea kocha huyo akaachana na Chelsea basi nyota huyo hatosajiliwa.

No comments:

Post a Comment