Chelsea yatoa sare, yavuna alama moja Klabu bingwa Ulaya - Darajani 1905

Chelsea yatoa sare, yavuna alama moja Klabu bingwa Ulaya

Share This

​Usiku wa jana kulichezwa mchezo wa hatua ya makundi ya Klabu bingwa barani Ulaya kwa soka la wana wake ambapo Chelsea ilishuka uwanjani kucheza mchezo wake wa kwanza kwenye hatua hiyo ndani ya msimu huu na ilicheza dhidi ya Wolfsburg ya nchini Ujerumani.


Mchezo huo uliisha kwa sare ya 3-3, uku Chelsea ilitoka nyuma kwa magoli 3-1 mpaka kusawazisha na kufanikiwa kuondoka na alama hiyo moja ikiwa nyumbani.


Magoli ya Chelsea yalifungwa na Samnatha Kerr ambaye alianza kuitanguliza Chelsea na kufanya ubao kusomeka 1-0 kabla ya Wolfsburg kusawazisha, kuongeza na kuongeza tena na kufanya ubao kusomeka 3-1, kisha Bethany England akasawazisha moja na ubao kusomeka 3-2 kabla ya baadae kabisa dakika za mwishoni, Pernille Harder ambaye alisajiliwa akitokea klabu hiyo ya Wolfsburg kufunga goli lililoipa Chelsea alama moja mara baada ya sare ya 3-3.


Matokeo hayo yanaifanya Chelsea kushika nafasi ya pili kutokana na kanuni za herufi ya kwanza, uku kundi likiongozwa na Juventus mwenye alama tatu ambaye yeye alama zake alizivuna mara baada ya ushindi wake wa mabao 3-0 dhidi ya Servette FCCF.




No comments:

Post a Comment