Klabu ya Real Madrid inatajwa kuwa tayari kumrudia winga wa Chelsea, Eden Hazard ambaye ilitajwa kumfukuzia toka dirisha kubwa la usajili lililopita ingawa Chelsea haikuwa tayari kumuachia winga wake huyo lakini sasa inadaiwa Chelsea ipo tayari kumuachia winga huyo ajiunge na Real Madrid lakini kwa sharti la kumtumia Gareth Bale kama nafasi ya dili hilo kama mabadilishano.
Mwandishi wa habari wa nchini Hispania, Eduardo Inda ameripoti kuwa Chelsea ipo tayari kuachana na Hazard lakini tu kama Real Madrid watamruhusu Gareth Bale ajiunge na Chelsea.
Chelsea imekuwa ikitajwa kwa muda mrefu kuhitaji huduma ya nyota huyo raia wa Wales kwa muda mrefu sana na sasa inataka kumnasa kwa kupitia dili au biashara ya Eden Hazard.
No comments:
Post a Comment