John Terry abadili mawazo, sasa anaitamani Chelsea - Darajani 1905

John Terry abadili mawazo, sasa anaitamani Chelsea

Share This

Alicheza Chelsea kwa mafanikio makubwa akiichezea kwa miaka 22 kabla ya kuachana nayo katika dirisha kubwa la usajili la msimu ujao, hakuwa tayari kustaafu soka lakini hakuwa tayari kucheza dhidi ya Chelsea akisema hawezi kucheza dhidi ya timu yake kipenzi na hivyo kukataa kujiunga na klabu kadhaa zinazoshiriki ligi kuu Uingereza akisema hataki kupambana dhidi ya Chelsea. Hatimaye akakubali kujiunga na klabu ya Aston Villa inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uingereza.

Sasa swali lipo je itakuwaje kama Aston Villa itafanikiwa kupanda kutoka daraja la kwanza (Championship) na kwenda ligi kuu Uingereza ambako huko ndiko ilipo timu yake kipenzi, Chelsea. Je atakubali kuendelea kuichezea Aston Villa ambayo ni lazima itacheza na Chelsea? John Terry amejibu swali hilo kupitia chombo cha habari cha talkSport ambapo amesema anatamani kuongeza mkataba wa kuitumikia Aston Villa kwa msimu mwengine na kama ikifanikiwa kufudhu kucheza ligi kuu Uingereza basi yupo tayari kucheza dhidi ya Chelsea.

"Chelsea itabaki kuwa klabu kipenzi kwangu lakini tangu nilipofika Aston Villa, nimepata mchango mkubwa kutoka kwa mashabiki. Walinikaribisha kwa mikono mikunjufu na napenda kujihisi kwa upendo walionikaribisha nao basi cha kuwalipa ni kufanya vizuri uwanjani na mazoezini"

"Tumekuwa na muunganiko mzuri na umekuwa ukifanya kazi vyema. Naliona hilo" alisema gwiji huyo aliyewai kuweka rekodi kadhaa pindi alipopita Chelsea.

Aston Villa kwa sasa ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi daraja la kwanza la Uingereza na itahitaji kucheza michezo ya ziada (play-offs) ili kufudhu kucheza ligi kuu Uingereza kwa msimu ujao.

No comments:

Post a Comment