Juventus waja na mpango mbadala wa kumnasa Morata - Darajani 1905

Juventus waja na mpango mbadala wa kumnasa Morata

Share This

Mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata anatajwa kuwa kwenye mipango ya kutakiwa na klabu ya nchini Italia, klabu ya Juventus ambayo aliwai kuichezea kabla ya kutua Chelsea.

Chombo cha habari cha Tuttosport kinadai Juventus imepeleka maombi ya kumsajili mshambuliaji huyo raia wa Hispania lakini wakija kwa nia ya kumsajili kwa mkopo wa miaka miwili. Klabu hiyo inatajwa kutokua tayari kulipa gharama za paundi milioni 60 ili kumsajili nyota, dau ambalo Chelsea ilitumia kumsajili akitokea Real Madrid lakini dau hilo linatajwa kutajwa na klabu ya Chelsea kama thamani ya mshambuliaji huyo.

Dau hilo la paundi milioni 60 linatajwa kuifanya Juventus kubadili mawazo na kumtaka mshambuliaji huyo kwa mkopo wa miaka miwili ambapo kutakuwa na kipengele cha kumsajili kabisa. Njia hiyo iliwai kutumika pia na Juventus kumnasa Juan Cuadrado kutoka Chelsea mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment