Mandzukic aiweka roho juu Chelsea - Darajani 1905

Mandzukic aiweka roho juu Chelsea

Share This

Klabu ya Juventus inayopatikana nchini Italia inaweza ikaachana na mshambuliaji wake, Mario Mandzukic ifikapo mwishoni mwa msimu huu ambapo jarida la Tuttosport la nchini humo linadai klabu yake ya Juventus ipo tayari kuachana na mshambuliaji wake huyo raia wa Croatia kama tu nyota huyo akitaka kuachana na klabu yake hiyo huku kukiwa na taarifa kuwa kuna klabu kutoka China na Uturuki tayari zishaonyesha nia ya kumtaka mshambuliaji huyo mwenye miaka 31 kwa sasa.

Lakini kama ikitokea kama mshambuliaji huyo akaachana na klabu hiyo, basi hiyo inaweza kuwa hatua mbaya kwa upande wa Chelsea.

Najua unajiuliza, Chelsea itaumia vipi wakati haijaonyesha nia ya kumtaka au hata haihusiki kwenye ofa ya mchezaji huyo. Ipo ivi, kuondoka kwa Mandzukic klabuni Juventus kutamaanisha klabu hiyo itahitaji kumpata mtu atakayerithi mikoba yake ambapo hapo kunaelezwa kuwa klabu hiyo itamfukuzia mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata.

Kiukweli Morata alishawai kukiri mara kadhaa kuwa ana mapenzi na klabu hiyo ya nchini Italia na kuna uwezekano siku moja akarejea kuichezea ambapo kuondoka kwa Mandzukic ni kama kutafungua milango kwa Morata kurejea klabuni hapo. Na kama unavyofahamu nchini Uingereza amekuwa akipata maneno mengi haswa kutoka kwenye vyombo vya habari wakihoji juu ya kiwango chake kushuka ambapo hiyo nayo inaweza kumfanya akatamani kuondoka Chelsea.

No comments:

Post a Comment