Kocha wa Chelsea, Antonio Conte bado haonekani kuwa na amani klabuni Chelsea ingawa amesaidia klabu hiyo kufika hatua ya nusu fainali ya kombe la FA lakini pia ikifufua matumaini ya kucheza klabu bingwa barani Ulaya kwa msimu ujao ambapo licha ya kufikia hapo alipo bado anahusishwa kuondoka klabuni Chelsea.
Thomas Tuchel haonekani tena kuwa mrithi wa kocha Antonio Conte klabuni hapo ambapo taarifa zinadai kuwa kocha huyo ameshafanya makubaliano na klabu ya PSG ili akaifundishe klabu hiyo inayotajwa kuachana na kocha wake wa sasa, Unai Emery.
Lakini gazeti jengine la huko nchini Uingereza limechapisha taarifa mpya ambapo linadai klabu hiyo inamtazamia kocha wake wa zamani, Brendan Rodgers ili airithi nafasi ya kocha Antonio Conte ifikapo mwishoni mwa msimu huu.
Brendan Rodgers ambaye ni raia wa Ireland uku akiwa anaifundisha klabu ya Celtic ya nchini Scotland anaweza kuwa mrithi wa kocha Antonio Conte ambaye anatajwa kutakiwa na timu ya taifa ya Italia.
Brendan aliwai kuifundisha klabu ya vijana ya Chelsea kuanzia mwaka 2004 mpaka mwaka 2008 lakini pia aliwai kuzifundisha klabu za Uingereza kama Swansea na Liverpool.
No comments:
Post a Comment