Eden Hazard aiongelea Chelsea kwa msimu ujao - Darajani 1905

Eden Hazard aiongelea Chelsea kwa msimu ujao

Share This

Chelsea ipo katika nafasi ya tano kwa sasa kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza huku ikiachwa kwa alama saba na Tottenham inayoshika nafasi ya nne kwenye msimamo huo huku kukiwa kumesalia michezo mitano kabla ya kumalizika kwa msimu wa 2017-2018 wa ligi kuu nchini Uingereza.

Ili Chelsea iweze kufudhu kucheza michuano ya klabu bingwa barani Ulaya msimu ujao, itatakiwa kumaliza ikiwa kwenye nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza na hilo litatimia kama Tottenham akipoteza alama nane kwenye alama 15 zilizobaki kwenye michezo hiyo mitano iliyobaki lakini Chelsea ikiwa imezivuna alama zote hizo 15 zilizosalia.

Nyota wa Chelsea, Eden Hazard ametoa neno na kuielezea Chelsea na nafasi yake ya kumaliza kwenye nafasi nne za juu ili iweze kufudhu kucheza klabu bingwa msimu ujao, nyota huyo alisema kikubwa ni kuhakikisha wanapambana kama timu ili kuweza kufanikiwa kushiriki klabu bingwa msimu ujao maana hata sasa wamejitoa sana na kupambana sana kama timu.

No comments:

Post a Comment