Wachezaji watano wa Chelsea watamba tunzo ya uchezaji bora - Darajani 1905

Wachezaji watano wa Chelsea watamba tunzo ya uchezaji bora

Share This

Klabu ya akinadada ya Chelsea, Chelsea Ladies imekuwa na msimu mzuri ikifanikiwa kuongoza katika msimamo wa ligi kuu Uingereza kwa akinadada lakini pia ikifanikiwa kufudhu kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya mara baada ya kuisambaratisha klabu ya Montpellier kwenye hatua ya robo fainali lakini pia jioni ya leo ipo uwanjani kucheza dhidi ya Manchester city Ladies.

Mara baada ya kuwa na msimu huo mzuri haswa kwa upande wa ligi kuu, kumetolewa orodha ya wachezaji wanaowania tunzo ya mchezaji bora wa mwaka (PFA Player of the year) ambapo Chelsea Ladies imefanikiwa kutoa nyota wake watano kati ya wachezaji sita wanaowania tunzo hiyo.

Mshambuliaji Fran Kirby ambaye amekua na msimu bora mpaka sasa akiifungia Chelsea magoli 21 kwa michuano yote ukijumlisha na goli alilolifunga hii leo dhidi ya Manchester city kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la FA kwa akinadada anawaongoza nyota wenzake ambao ni Ji So Yun, Ramona Bachmann, Millie Bright pamoja na Mjelde ambao wote wanapambania tunzo hiyo ya mchezaji bora wa mwaka.

Hongereni akinadada wa Chelsea Ladies..

No comments:

Post a Comment