Fran Kirby aifikisha Chelsea fainali kombe la FA - Darajani 1905

Fran Kirby aifikisha Chelsea fainali kombe la FA

Share This

Chelsea Ladies inafanikiwa kutinga fainali katika kombe la FA mara baada ya jioni ya leo kupata ushindi wa mabao 2-0 wakiwa nyumbani Kingsmeadow wakiibaragaza klabu ya Manchester city Ladies.

Mpaka kumalizika kwa kipindi cha kwanza, Chelsea Ladies ilikuwa mbele kwa goli 1-0 ambapo goli hilo lilifungwa na nyota wake Fran Kirby ambaye amefanikiwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha mchezaji bora wa mwaka uko nchini Uingereza.

Fran Kirby aliifungia tena Chelsea goli la pili katika dakika ya 74 na kuifanya Chelsea Ladies kuondoka na ushindi wake muhimu katika hatua hiyo ya nusu fainali huku goli hilo likiwa goli lake la 22 kwa michuano yote kwenye msimu huu.

Chelsea Ladies itacheza fainali ya kombe hilo la FA dhidi ya Arsenal Ladies tarehe 5-May mwaka huu.

No comments:

Post a Comment