Nyota wa Chelsea aipa ubingwa klabu ya Uholanzi - Darajani 1905

Nyota wa Chelsea aipa ubingwa klabu ya Uholanzi

Share This

Nyota wa Chelsea anayeichezea kwa mkopo klabu ya PSV ya nchini Uholanzi, Marco van Ginkel amefanikiwa kuisaidia klabu hiyo ya nchini huko kutwaa ubingwa wake wa ligi kuu nchini Uholanzi.

van Ginkel mwenye miaka 25 amefanikiwa kuisaidia timu hiyo kushinda taji hilo la ligi kuu mara baada ya kufikisha alama 80 huku ikiiacha Ajax kwa alama 10 huku ikiwa imesalia michezo mitatu kabla ya kumalizika kwa ligi kuu hiyo ya nchini humo.

van Ginkel ameichezea kwa jumla ya michezo 31 huku akiifungia magoli 16 na kutengeneza mengine manne.

Hongera kwake Marco van Ginkel..

No comments:

Post a Comment