Nyota wa Chelsea anayeichezea kwa mkopo klabu inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza, klabu ya Newcastle, Kenedy amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Marchi kwenye klabu yake hiyo anayoichezea kwa mkopo.
Nyota huyo aliyeungana na klabu hiyo kwa mkopo kwenye dirisha la usajili la mwezi Januari ameshinda kinyang'anyiro hicho na kuwa mchezaji bora wa mwezi uliopita mara baada ya kushinda kwa asilimia 58 ya kura zilizopigwa kwenye mtandao wa klabi hiyo huku akiwapiku wapinzani wake.
Kenedy ameshaichezea Newcastle michezo 9 huku akiifungia magoli 2 na kutengeneza mengine mawili.
Hongera Kenedy..
No comments:
Post a Comment