Alizaliwa mwaka 1998 na mpaka sasa bado miezi kadhaa ili atimize miaka 20 toka kuzaliwa kwake, ni kiungo imara kwenye kikosi cha klabu ya soka ya akinadada ya Chelsea, Chelsea Ladies huku akihusika vyema kwenye mafanikio ya klabu hiyo toka atue akitokea klabu ya nchini kwao Scotland na kutua Chelsea Ladies mwaka 2017. Ni Erin Cuthbert.
Nyota huyo amehusika vyema kwenye mafanikio ya kikosi hicho kilichochini ya kocha Emma Hayes na hivyo kuchaguliwa kuwa mmoja wa wachezaji watakaowania tunzo ya mchezaji bora chipukizi kwa soka la akinadada kwa ligi kuu Uingereza.
Erin Cuthbert ameingia kwenye kinyang'anyiro cha kugombania tunzo hiyo inayotolewa na PFA kwa ligi kuu Uingereza ambapo kwa upande wa soka la wanawake Chelsea Ladies imefanya vizuri ambapo vita ya kugombania ubingwa wa ligi kuu nchini humo ikiwa ya klabu mbili yaani Chelsea Ladies na Manchester city Ladies.
Hongera Erin Cuthbert..
No comments:
Post a Comment