Nyota wa Chelsea apatwa na majanga makubwa - Darajani 1905

Nyota wa Chelsea apatwa na majanga makubwa

Share This

Nyota wa Chelsea anayeichezea kwa mkopo klabu ya Borrusia Dortmund ya nchini Ujerumani, Michy Batshuayi amepata majeraha kwenye mchezo wa ligi kuu nchini humo dhidi ya Schalke 04.

Katika mchezo huo ulioisha kwa Dortmund kupoteza kwa magoli 2-0 wakiwa ugenini, Michy alipata majeraha katika dakika ya 92 wakati akiwania mpira na mchezaji wa timu pinzani ndipo akaanguka na kupata majeraha kwenye kifundo cha mguu na kumfanya kukimbizwa hospitalini haraka.

Mara baada ya mchezo, kocha wa Dortmund alisema kwa muda huo hajui hali aliyokuwa nayo nyota huyo lakini akidai ni kweli nyota huyo alitolewa akiwa na maumivu makali na kuna wasiwasi kuwa amepata majeraha makubwa yanayoweza kumfanya kuwa nje kwa muda mrefu.

Majeraha hayo yanaweza kumfanya nyota huyo raia wa Ubelgiji kuzikosa fainali za kombe la dunia zinazotarajiwa kufanyika mwezi Juni huko nchini Urusi.

No comments:

Post a Comment