Klabu yetu pendwa ya Chelsea haionekani kuwa na mpango wa kuendelea na kocha wake wa sasa raia wa Italia, Antonio Conte kwa msimu ujao, mara baada ya kocha huyo kushindwa kuipatia mafanikio makubwa mara baada ya msimu uliopita kuisaidia kushinda taji la ligi kuu Uingereza.
Kuna makocha wengi wanatajwa kuwaniwa na Chelsea ili kuziba nafasi ya kocha huyo pindi atakapoachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu licha ya kubakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wa sasa ambao aliusaini mara baada ya kuisaidia klabu hiyo kushinda taji hilo la ligi kuu kwa mwaka jana.
Massimiliano Allegri ambaye ni kocha wa Juventus anatajwa pia kama mmoja wa makocha wanaowaniwa na Chelsea ili arithi mikoba ya muitaliano mwenzake kwa mara nyengine tena ambapo ilishawai kutokea hivyo kwa Allegri kuchukua nafasi ya Conte kwenye klabu ya Juventus au vibibi vizee vya Turin.
"Nina mkataba hapa mpaka mwaka 2020 na nina furaha ya kubaki hapa. Nina wakati mzuri na klabu yangu. Pindi dirisha la usajili linapofunguliwa huwa sishughuliki sana na swala la usajili maana naiamini klabu yangu"
"Bado tunahitaji kuyafikia malengo na madhumuni yetu. Kama hatutoshinda Scudetto (Ligi kuu Italia) na Coppa Italia (Kombe la Italia) bado haitosababisha wao kunikataa. Tutakaa chini na kuzungumza jinsi ya kufanya kama tulivyokua tunafanya kwa miaka mingine" alisema kocha huyo.
Lakini kwa maneno haya umeelewa jambo gani? kuna vuguvugu linaendelea klabuni Chelsea ambapo kocha Antonio Conte amekuwa akilalamika hadharani juu ya bodi ya klabu hiyo inavyofanya usajili huku akidai amekua hashirikishwi kwa kiasi kikubwa kama kocha mkuu na hilo limekuwa gumzo na ndio maana hata Allegri ameongelea juu ya kuiamini bodi ya klabu yake.
Usajili klabuni Chelsea unasimamiwa na bodi ya Chelsea ambapo bodi hiyo ina mamlaka ya kufanya usajili wa kununua au kuuza mchezaji yoyote klabuni hapo huku mamlaka hayo yakisimamiwa na mwanamama Marina Glanovskaia ambapo kwa mfumo huo, kocha Antonio Conte amekuwa akilalamika mara kwa mara kuwa hashirikishwi kwenye kufanya maamuzi juu ya wachezaji wa kuwasajili au kuwauza.
Hili kalitamka Allegri tu, vipi na hao makocha wengine wanaotajwa kutakiwa na Chelsea? Luis Enrique, Brendan Rodgers wa Celtic na wengine wengi, je wanafurahishwa na mtindo wa usajili unavyofanyika Chelsea? Jibu ni Hapana, kila kocha anapenda kuletewa mchezaji aliye kwenye mahesabu yake.
No comments:
Post a Comment