Kati ya maswali ambayo kocha Antonio Conte amekuwa akiulizwa akifanya mikutano au mahojiano na waandishi wa habari basi ni kuhusu mustakabali wake wa kubaki kuwa kocha wa Chelsea kwa msimu ujao, ambapo waandishi wengi wamekuwa wakiripoti kuwa kocha huyo hana furaha ya kubaki klabuni hapo haswa kutokana na kutokufurahishwa na mfumo wa usajili unavyofanyika ambapo usajili wote unaamriwa na bodi ya klabu hiyo inayoongozwa na mwanamama Marina Glanovskaia.
Lakini nyakati zote ambazo swali hilo amekuwa akikutana nalo hajawai kusita na kukiri anafuraha na anapenda kubaki klabuni Chelsea ingawa anatambua klabu hiyo haina kariba ya kukaa na makocha kwa muda mrefu.
Kuonyesha kwa kiasi gani anapenda kuendelea kubaki Chelsea, kocha huyo amewapa funzo wachezaji wa klabu hiyo juu ya kipindi iki ambacho kinaonekana kuwa kibaya kwa Chelsea inayoshika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza huku ikiwa imebakiza taji moja tu la kombe la FA ambalo ina nafasi ya kulitwaa.
"Niliwai kuwa mchezaji, na kuwa mchezaji ni lazima ucheze kila mchezo, sio kwa ajili yangu kama kocha ila kwa ajili ya klabu na mashabiki"
"Wanatakiwa waiheshimu hii nembo (ya Chelsea), hawatakiwi kucheza kwa heshima ya kocha. Wanatakiwa wacheze kwa ajili ya klabu na mashabiki wetu na kuonyesha kwa kiasi gani wanawajibika. Hiyo ndio njia pekee ya mchezaji kuwa bora na kuitwa mchezaji bora" alisema kocha huyo muitaliano.
No comments:
Post a Comment