Batshuayi akutwa na majanga - Darajani 1905

Batshuayi akutwa na majanga

Share This

Dakika ya 90+2' ya mchezo alipata majeraha mara baada ya kugombania mpira na mlinzi wa Schalke 04 ambapo alipata maumivu yaliyomfanya ashindwe kumalizia mchezo huku akikimbizwa hospitalini ambapo mpaka mchezo unaisha haikujulikana hali yake inaendeleaje.

Ni mshambuliaji wa Chelsea, Michy Batshuayi ambapo jana alikutwa na kadhia hiyo akiichezea klabu ya Borrusia Dortmund ambapo aliungana na klabu hiyo kuichezea kwa mkopo.

Mara baada ya kusubiri kwa muda, hatimaye majibu yametoka juu ya ajali hiyo aliyokutana nayo ambapo majibu yanasema nyota huyo hatoweza kuendelea na soka mpaka msimu kuisha.

Batshuayi aliyepata majeraha hayo ya enka katika mchezo huo wa ligi kuu Ujerumani ambapo Dortmund ilipoteza kwa magoli 2-0 ikiwa ugenini hatorejea tena uwanjani na badala yake atatumia msimu uliobaki akiuguza majeraha.

No comments:

Post a Comment