Huenda akawa hatajwi sana, au jina lake kuzungumzwa sana juu ya kurithi nafasi ya kocha wa Chelsea wa sasa, Antonio Conte, lakini kati ya majina yanayohusishwa kutua klabuni hapo na kuifundisha klabu ya Chelsea mara baada ya msimu huu kuisha.
Ni Thomas Tuchel, kocha wa zamani wa klabu ya Borrusia Dortmund ambaye inaelezwa kwa sasa hana timu anayoifundisha licha ya kuwepo taarifa zinazoaminika kuwa kocha huyo amekataa kuifundisha klabu ya Bayern Munich iliyompelekea ombi la kumuajiri kocha huyo mara baada ya msimu huu kuisha.
Taarifa zilizopo zinadai kocha huyo amekataa kuajiriwa na Bayern Munich, taarifa inayozifanya klabu za Chelsea na Arsenal kukaa mkao wa kula ili kumnasa kocha huyo.
Taarifa hizo zinadai Thomas Tuchel yupo kwenye mipango ya kutakiwa na klabu kadhaa ikiwemo klabu ya Chelsea inayohusishwa kutaka kumuuza kocha wake Antonio Conte. Sio Tuchel tu anayetajwa kutakiwa na Chelsea, wengine ni kama Luis Enrique na Maurizio Sarri ambaye naye anatajwa kufikia hatua za mwisho kabla ya kusaini mkataba mpya na klabu yake ya Napoli.
No comments:
Post a Comment