Kocha wa zamani wa Borrusia Dortmund, Thomas Tuchel ambaye kwa sasa hana timu anayoifundisha mara baada ya kuachana na klabu hiyo, amekuwa akitajwa kutakiwa na klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani kabla ya chanzo cha kuaminika kutoa taarifa kuwa kocha huyo ameikataa klabu hiyo na sasa anatazamwa kama anaweza kuwa mrithi wa kocha Antonio Conte klabuni Chelsea.
Taarifa hiyo ya kocha huyo kutakiwa na Chelsea ni kama imeibuka katika siku mbili hizi, na ni kama imekuwa taarifa nzuri kwa mashabiki wengi wa Chelsea ambapo kupitia mtandao wa Twitter na maoni yaliyoulizwa kwa mashabiki wa Chelsea, wengi wao wanaonekana kufurahishwa na klabu yao kumtaka kocha huyo mwenye miaka 44 kwa sasa huku akitajwa kutakiwa na klabu ya Arsenal.
Taarifa zilizopo zinaeleza mashabiki wengi wa Chelsea wanatamani kama klabu yao ikiamua kumtimua Antonio Conte anayetajwa kutakiwa pia na klabu ya PSG na timu ya taifa ya Italia basi Thomas Tuchel ndiye anafaa kurithi majukumu ya kocha huyo klabuni Chelsea.
No comments:
Post a Comment