Chelsea inashika nafasi ya tano kwa sasa kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza ikiachwa alama chache na Tottenham wanaoshika nafasi ya nne kwenye msimamo huo, huku mwisho wa wiki hii klabu hizo zitashuka uwanjani kumenyana pale Stamford Bridge, Darajani.
Kuelekea kwenye mchezo huo, kocha Antonio Conte anahitaji kuhakikisha Chelsea inapata ushindi muhimu dhidi ya klabu hiyo inayofundishwa na kocha Mauricio Pochettino.
Mchambuzi wa soka, Ray Wilkins ambaye aliwai kuwa mchezaji na kocha msaidizi wa Chelsea amemshauri kocha Antonio Conte jinsi ya kupanga kikosi ili kuweza kupata alama tatu muhimu katika mchezo huo wa watani wa jadi wanaopatikana London wote.
"Chelsea inatakiwa kuifanya Tottenham ipate tabu. Kama itahitaji kufanya hivyo basi naamini Fabregas na Kante watakuwa ni watu sahihi kucheza katika nafasi ya kiungo" alisema gwiji anayefanya kazi ya uchambuzi kwa sasa.
Chelsea itashuka uwanjani hapo huku ikiwa na historia nzuri dhidi ya Tottenham ambapo katika michezo mitano ambayo Chelsea imekuwa chini ya kocha Antonio Conte, basi imeshinda michezo minne na kupoteza mchezo mmoja huku mchezo uliopita uliokuwa wa ligi kuu uliochezwa kwenye uwanja wa Wembley ambao unatumiwa na Tottenham kama uwanja wake wa nyumbani, Chelsea ilishinda 2-1 huku magoli ya Chelsea yakifungwa na Marcos Alonso.
No comments:
Post a Comment