Asensio awaonya Madrid, Chelsea yamkaribia - Darajani 1905

Asensio awaonya Madrid, Chelsea yamkaribia

Share This

Chelsea inahusishwa kuwa tayari kumsajili nyota wa klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania, Marco Asensio ambaye nae ni raia wa nchini humo ambapo inatajwa kuwa tayari kutoa dau nono ili kumnasa nyota huyo mwenye miaka 22 ingawa klabu yake inaonekana kutokua tayari kumuuza kinda wake huyo mwenye kipaji cha hali ya juu.

Lakini pia gazeti la nchini Hispania limekuja na taarifa mpya ambapo linadai nyota huyo ambaye aliingia katika kipindi cha pili katika mchezo wa klabu bingwa barani Ulaya ambapo Real Madrid ilicheza dhidi ya Juventus ambapo jambo hilo la kuonekana kutotumika katika kikosi cha kwanza linadaiwa kumfanya nyota huyo kuwafata viongozi wa Real Madrid na kuwaambia kama watataka asalie klabuni hapo basi ahakikishiwe nafasi kwenye kikosi hicho lakini pia asisajiliwe mchezaji mwengine anayecheza kwenye nafasi anayocheza mwenyewe.

Chelsea kupitia kwa mmiliki wake, Roman Abramovich inatajwa kutamani kuwa na huduma ya nyota huyo huku ikielezwa mmiliki huyo yupo tayari kutoa fungu nono ili kumnasa mhispania huyo.

No comments:

Post a Comment