Loftus-Cheek aeleza nini anakiwaza kuhusu Chelsea - Darajani 1905

Loftus-Cheek aeleza nini anakiwaza kuhusu Chelsea

Share This

Alijiunga kwa mkopo katika klabu ya Crystal Palace katika dirisha kubwa la usajili la kipindi cha kiangazi ambapo baadae alipata majeraha yaliyomfanya kurudishwa kwenye klabu inayommiliki ya Chelsea ambapo huko alifanyiwa matibabu ili kuwekwa sawa kiafya na siku kadhaa zilizopita alirejea Crystal Palace na hata aliichezea mchezo uliopita ambapo Crystal ilicheza dhidi ya Brighton & Hove Albion.

Ni kiungo wa Chelsea raia wa Uingereza, Ruben Loftus-Cheek ambaye kwa sasa yupo chini ya kocha mkongwe, Roy Hodgson kwenye klabu hiyo ya Crystal Palace amefanyiwa mahojiano na kuulizwa ni jambo gani analoliwaza au kulifikiria kwa sasa juu ya kurejea kwake Chelsea, sehemu ambayo hakupata muda mwingi wa kucheza au asalie na klabu hiyo ya Crystal Palace ambapo kuwa kwake hapo kunamfanya apate muda mrefu wa kucheza soka.

"Kiukweli kwa sasa sifikirii lolote kati ya kuondoka hapa na kurejea Chelsea au hata kuendelea kubaki hapa. Kikubwa nachokiwaza na kukifikiria ni jinsi gani ya kuisaidia klabu yangu ya sasa kuipa mafanikio kwenye hii michezo iliyobaki"

"Kama kusalia hapa au kurudi Chelsea nadhani hilo nitaliamua muda ukishawadia. Sikuwai kupambana kama hivi navyopambana kwa sasa, unaonja radha ya kila mchezo kwa kupambana kila mwisho wa wiki, ukipambania alama tatu, ni jambo zuri kwa kila mchezaji kuhusika kwenye kila mchezo wa ligi kuu" alisema nyota huyo mwenye miaka 22 kwa sasa.

Ruben Loftus Cheek ni zao la Chelsea ambapo alilelewa na kukuzwa na akademi ya Chelsea huku akipata sifa nyingi kutoka kwa wachambuzi wengi juu ya aina ya soka analocheza huku akiwavutia wengi katika uwezo mkubwa wa kutoa pasi.

No comments:

Post a Comment