Tunzo ya mchezaji bora wa Chelsea, piga kura hapa - Darajani 1905

Tunzo ya mchezaji bora wa Chelsea, piga kura hapa

Share This

Tarehe 10-May mwaka huu kutakuwa na tukio maalumu linaloihusu klabu yetu pendwa ya Chelsea ambapo kutafanyika shughuli kubwa na muhimu kwa klabu hiyo, shughuli ya kutolewa kwa tunzo za waliofanya vyema kwa msimu mzima wa 2017-2018 katika michuano yote ambayo Chelsea imeshiriki katika msimu huu wote.

Tunzo tatu zitatolewa kwa wachezaji hao wa Chelsea ambazo ni tunzo za Mchezaji bora wa mwaka au msimu (Best player of the year), Mchezaji bora kwa wachezaji (Best players' player of the year) na goli bora la msimu (Goal of the season).

Mimi mwandishi wako nishapiga kura yangu kumchagua mchezaji bora niliyeona anastahili kushinda tunzo hiyo kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa msimu mzima tukiwa tunaelekea mwishoni mwa msimu.

Nawe kama upo tayari kupiga kura yako kumchagua mchezaji unayodhani anastahili kushinda tunzo hiyo, basi bonyeza hapa

NB; Kwa tunzo ya goli bora la msimu (Goal of the season) nitakuletea hivi punde

No comments:

Post a Comment