Kocha wa Chelsea atoa neno kucheza fainali ya kombe la FA - Darajani 1905

Kocha wa Chelsea atoa neno kucheza fainali ya kombe la FA

Share This

Klabu ya soka ya wanawake ya Chelsea Ladies inafanikiwa kupata ushindi muhimu inayoifanya iweze kufudhu kucheza fainali ya kombe la FA ambapo itacheza dhidi ya Arsenal Ladies siku ya tarehe 5-May kwenye uwanja wa Wembley uliopo London.

Magoli mawili ya Fran Kirby ndiyo yaliyosaidia Chelsea kufikia hatua hiyo kwa mara ya tatu katika misimu minne, lakini kwenye mchezo huo Chelsea Ladies iliwakosa nyota wake kama Ji So-Yun ambaye alikuwa akiitumikia timu yake ya taifa lakini pia kwa nyota wengine walikuwa wakiuguza majeraha. Kocha mkuu wa kikosi hicho, Emma Hayes akatoa neno juu ya ushindi huo muhimu kwa Chelsea.

"Tumekuwa na wiki yenye changamoto nyingi. Baadhi ya wachezaji tumeshindwa kuwa nao kutokana na shida binafsi wakati wengine wakiwa wanauguza majeraha"

"Imekuwa ni wiki ngumu kutokana na wachezaji kutoka kwenye michezo ya kimataifa lakini hatuna sababu ya kusingizia, tumewatumia wale waliopo. Muda mwingine unapambana sana mazoezini ukiwa na nguvu ndogo lakini inatakiwa ujiandae kwa matukio makubwa. Huu ni ushindi kwa wale waliotumika na kupambana uwanjani lakini pia ni ushindi kwa wale waliokosekana. Nakiamini kikosi changu" alisema kocha huyo.
*************
Kama unataka kupiga kura ili kumchagua mchezaji unayedhani anastahili kushinda tunzo ya mchezaji bora wa msimu wa 2017-2018 kwa klabu ya Chelsea, basi bonyeza hapa

No comments:

Post a Comment