Ilikuwa ni moja ya matukio yaliyoacha gumzo kwenye mchezo uliopita wa Chelsea dhidi ya Southampton ambapo Chelsea ilikuwa ugenini na kupata ushindi muhimu wa mabao 2-3 kwenye uwanja wa St. Mary mara baada ya nyota wa Chelsea, Marcos Alonso kumkanyaga kwa bahati mbaya mchezaji wa timu pinzani wakati wanawania mpira, tukio ambalo wachambuzi wengi wa soka walimkosoa mwamuzi wa mchezo huo, Mike Dean kwa kushindwa kumpa kadi nyekundu Marcos Alonso.
Lakini kwa habari zilizopo zinadai, chama cha soka nchini Uingereza, FA kupitia kitengo maalumu kwa matukio kama hayo yanafanya uchunguzi juu ya tukio hilo na kama ikibainika Marcos Alonso alifanya makusudi basi watampa adhabu sawa na mtu aliyepata kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kufungiwa michezo mitatu.
Kama akifungiwa michezo hiyo mitatu basi ataikosa michezo ya ligi kuu miwili dhidi ya Burnley utakaochezwa kesho kutwa tarehe 19-Aprili pamoja na dhidi ya Swansea lakini pia ataukosa mchezo wa nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Southampton utakaochezwa jumapili ya wiki hii, yaani tarehe 22-Aprili.
No comments:
Post a Comment