Drinkwater aibua mzozo mkubwa Chelsea - Darajani 1905

Drinkwater aibua mzozo mkubwa Chelsea

Share This

Chelsea ilimsajili akitokea Leicester city kwa dau la paundi milioni 35 katika dirisha kubwa la usajili lililopita huku akitegemewa kufanya makubwa akiwa sambamba na kiungo mwenzake, N'Golo Kante ambae walitamba wakiwa pamoja walipoisaidia Leicester kutwaa ubingwa wa ligi kuu Uingereza kwa msimu wa 2015-2016.

Danny Drinkwater anatajwa kutokua na furaha ya kuendelea kusalia kuwa nyota wa Chelsea mara baada ya kutopata muda wa kucheza zaidi huku klabu ya West Ham ikitajwa kuvutiwa na huduma yake.

Gazeti la talkSport linadai klabu ya Chelsea inakaribia kumpoteza mwingereza huyo amedumu Chelsea kwa msimu mmoja huku akiichezea michezo 23 na kuifungia goli moja kwa michuano yote ndani ya msimu huu anatajwa kutakiwa kwa uhudi na uvumba na klabu ya West Ham.

Ripoti zinadai West Ham inakaribia kumsainisha moja ya viongozi kutoka Leicester city ambapo wanajua wakifanikiwa kumpata kiongozi huyo basi watafanikiwa kumnasa Drinkwater ambaye kwa sasa ana miaka 28.

Kocha Antonio Conte alihojiwa kabla ya mchezo uliopita kati ya Chelsea dhidi ya Southampton juu ya kiungo huyo kutokuwa na amani klabuni Chelsea na kocha Antonio Conte alijibu akisema " Tunamzungumzia mchezaji mzuri, ila amekuwa na msimu mbaya kutokana na majeraha aliyoyapata na kumfanya akae nje. Ni mchezaji bora, nami namuamini" alisema kocha huyo.

No comments:

Post a Comment