Miaka 30 iliyopita siku kama ya leo alizaliwa mwanasoka mmoja huko nchini Uingereza ambaye kwa sasa anatamba na klabu ya soka ya wanawake, klabu ya Chelsea Ladies, ni Gemma Suzanne Davison ambaye leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.
Alisajiliwa na Chelsea Ladies akitokea Liverpool Ladies huku akiwa na uwezo mkubwa wa kucheza nafasi ya winga wa kulia lakini pia akicheza kama winga mkabaji (wing-back) huku akiisaidia Chelsea kushinda mataji kadhaa.
Leo.anatimiza miaka 30 na bado ni mchezaji muhimu kwenye kikosi cha kocha Emma Hayes ambacho kimekuwa na mafanikio makubwa kwa misimu mfululizo.
Nasi kama mashabiki wa Chelsea tunasema hongera kwake na heri ya kuzaliwa kwa nyota huyu.
No comments:
Post a Comment