Nyota wa Bayern Munich kumtimua Morata kutoka Chelsea - Darajani 1905

Nyota wa Bayern Munich kumtimua Morata kutoka Chelsea

Share This

Nyota wa Chelsea, Alvaro Morata anatajwa kuwa kwenye mipango ya kutakiwa na klabu ya nchini Italia, klabu ya Juventus, klabu ambayo aliwai kuichezea kabla ya kutua Darajani.

Lakini gazeti mojawapo la nchini Hispania ambalo ni taifa la nyota huyo, gazeti la Don Balon limeripoti Chelsea itakuwa tayari kuachana na mshambuliaji huyo endapo itafanikiwa kumnasa nyota wa Bayern Munich ya nchini Ujerumani, Robert Lewandowski ambaye anatajwa kutakiwa pia na klabu ya Real Madrid.

Taarifa hizo zinadai Chelsea ipo tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 86 ambacho kinatakiwa na klabu yake ya Bayern Munich na endapo itafanikiwa kumnasa basi itafungua milango kwa Juventus kufanya mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji huyo aliyesajiliwa kwa dau la paundi milioni 60 akitokea Real Madrid.

No comments:

Post a Comment