Ji kucheza kombe la dunia 2019 - Darajani 1905

Ji kucheza kombe la dunia 2019

Share This

Nyota wa Chelsea Ladies ambayo ni klabu ya soka ya wanawake, Ji So-Yun hakuwepo wakati Chelsea Ladies ilipoibamiza Manchester city Ladies kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la FA ambapo mchezo huo uliisha kwa Chelsea Ladies kuondoka na ushindi wa mabao 2-0, ushindi ambao unamaanisha Chelsea itacheza fainali ya michuano hiyo.

Kukosekana kwa nyota huyo kulitoa kutokana na nyota huyo kuwa na majukumu na timu yake ya taifa ya Korea ya Kusini ambao walikuwa na mchezo wa kugombania nafasi ya kucheza kombe la dunia kwa wanawake litakalochezwa mwaka 2019 huko nchini Ufaransa.

Na hatimaye timu hiyo ikafanikiwa kufudhu mara baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya timu ya Ufilipino. Huku nyota huyo akicheza kwa kiwango cha hali ya juu kabla ya kufanyiwa mabadiliko dakika ya 72 wakati timu yake ikiwa mbele kwa magoli 4-0.

Mara baada ya ushindi huo, timu hiyo imekata tiketi ya kucheza kombe la dunia mwakani huko nchini Ufaransa.

Hongera Ji So-Yun ambaye pia anagombania tunzo ya uchezaji bora wa msimu wa 2017-2018.

No comments:

Post a Comment