Chelsea yaiwekea mtego Dortmund kwa Batshuayi - Darajani 1905

Chelsea yaiwekea mtego Dortmund kwa Batshuayi

Share This

Amekuwa na kiwango bora tangu ajiunge kwa mkopo kwenye klabu ya Borrusia Dortmund akitokea Chelsea, mpaka sasa ameshaichezea klabu hiyo michezo 14 huku akiifungia magoli 9 kabla ya kupata majeraha kwenye mchezo wake wa mwisho dhidi ya Schalke 04 ambapo Dortmund ilipoteza kwa magoli 2-0 huku nyota huyo raia wa Ubelgiji akipata majeraha yaliyomfanya kukimbizwa haraka hospitalini ambapo baadae majibu yalitoka yakisema nyota huyo hatoweza kurejea uwanjani kuichezea Dortmund kutokana na majeraha hayo kutarajiwa kupona wakati msimu ukiwa ushaisha.

Ni Michy Batshuayi, nyota wa kibelgiji mwenye miaka 24 kwa sasa, inaelezwa kuwa Chelsea imekubali kumuuza nyota huyo kwa klabu hiyo anayoitumikia kwa mkopo utakaoisha mwishoni mwa msimu huu.

Chelsea inatajwa kuweka kiwango cha paundi milioni 50 kwa mshambuliaji huyo kama kuna klabu itahitaji huduma yake. Klabu ya Dortmund kupitia kwa rais wake iliwai kuripotiwa kujaribu kumsajili lakini Chelsea ikagoma kumuuza lakini inahisiwa kutokana na majeraha yake yameifanya klabu hiyo kubadili mawazo na kukubali kumuuza.

Kama Chelsea ikifanikiwa kumuuza mbelgiji huyo, basi itakuwa imefanikiwa kutengeneza faida ambapo yenyewe ilimsajili kwa paundi milioni 35 akitokea Olympique Marseille ya Ufaransa.

No comments:

Post a Comment